Storm FM

Vifaa vya matibabu vya milioni 400 vyanunuliwa Nyang’hwale

31 October 2023, 7:49 pm

Moja ya kifaa cha matibabu cha kisasa katika Hospitali ya wilaya ya Nyang’hwale. Picha na Mrisho Sadick

Serikali imedhamilia kuboresha huduma za afya kwa kujenga nakupeleka vifaa vya kisasa vya matibu katika Zahanati , Vituo vya afya na Hospitali.

Na Mrisho Sadick – Geita

Serikali imetoa zaidi ya milioni 400 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa  katika Hospitali ya wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita ili kurahisisha utolewaji wa huduma za kibingwa wilayani humo.

Mganga Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale Dkt Nevelin Mwakabuku amesema hayo katika zoezi la kuwapokea madaktari Bingwa Kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato watakao kuwa katika hospitali hiyo kwa siku tano kwa ajili ya kutoa huduma za kibingwa bure kwa wananchi.

Sauti ya Mganga Mkuu Nyang’hwale
Viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale wakiwa na madaktari kutoka Hosptali ya Rufaa ya Kanda Chato. Picha na Mrisho Sadick

Kwa upande wake Dkt Gerald Samson daktari wa magonjwa ya watoto kutoka Hosptali ya kanda Chato amesema uwepo wao katika hosptali ya wilaya ya Nyang’hwale kwa siku tano utawasaidia wananchi kupata matibabu bure pamoja nakuwajengea uwezo watumishi wa hospitali hiyo.

Sauti ya Dkt Samson Hospitali ya Rufaa ya kanda Chato

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale Husna Tony amewataka wakazi eneo hilo kutumia Hospitali hiyo huku Katibu tawala wa wilaya hiyo Kaunga Omary amewatoa wasiwasi wananchi Juu ya huduma zinazotolewa katika eneo hilo.

Sauti ya Mkurugenzi wa Halmashauri na Katibu tawala wilaya ya Nyang’hwale
Huduma za matibabu kwa wananchi zikiendelea katika Hospitali ya wilaya ya Nyang’hwale. Picha na Mrisho Sadick