Storm FM

TUWALEE KWA PAMOJA yasaidia wahitaji mjini Geita

25 June 2024, 11:45 am

Wanakikundi cha TUWALEE wakiwa nje ya gereza la wilaya ya Geita mara baada ya kutembelea. Picha na Edga Rwenduru

Kikundi cha TUWALEE kilichopo mjini Geita kimetoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa makundi ya watu wenye uhitaji mkoani Geita.

Na: Edga Rwenduru – Geita

Kikundi hicho chenye zaidi ya wanawake 30 ambao ni wafanyabiashara na wajasiriamali kimetoa msaada huo Juni 23, 2024.

Wanakikundi cha TUWALEE wakiwa na baadhi ya mahitaji waliyotoa kwa wahitaji. Picha na Edga Rwenduru

Wahitaji waliotembelewa ni wale waliopo katika gereza la wilaya ya Geita, kituo cha kulelea watoto yatima cha Bright Light Organization, familia zenye uhitaji zisizopungua kumi zilizopo kata ya Bombambli pamoja na kutembelea wodi ya wazazi na watoto katika hospitali ya halmashauri ya mji Geita.

Mwenyekiti wa kikundi hicho Irene Okololo amesema huo ni mwanzo na kwamba zoezi hilo litakuwa endelevu kila mwaka huku akitaja baadhi ya vitu ambavyo wametoa kwa wahitaji

Sauti ya mwenyekiti
Baadhi ya mahitaji waliyopatiwa watu wenye uhitaji. Picha na Edga Rwenduru

Akizungumza mara baada ya kikundi hicho kufika hospitali ya halmashauri ya mji, mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Geita Dkt. Sunday Mwakyusa amesema idadi kubwa ya watoto wanaokaa muda mrefu hospitali wakiwa wanaumwa ni wale wenye utapiamulo.

Sauti ya mganga mkuu