Storm FM

GGML yaipa donge nono Geita Gold FC

17 December 2022, 2:37 pm

Na Zubeda Handrish:

Kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Geita Golid Mining Limited (GGML) @anglogoldashantitanzania imeingia udhamini kwa mara nyingine tena na Geita Gold Football Club kwa mkataba mnono wa thamani ya Sh. Milioni 800 kwa mwaka 2022/2023.

Kufuatia mkataba huo unaifanya GGML kuendelea kuwa mdhamini Mkuu wa @geitagoldfc na kuendelea kuifanya timu hiyo kushiriki kikamilifu katika ligi kuu ya Tanzania Bara kwa Msimu wa Ligi 2022-2023 na Shughuli zingine za kimaendeleo za klabu hiyo.

Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Zahara Michuzi ameushukuru mgodi huo na kuahidi makubwa kutoka katika klabu hiyo huku mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Willison Shimo akitoa pongezi kwa mgodi wa GGML kwa kuonesha uzalendo.