Storm FM

Shamrashamra Simba Day zaendelea Senga

7 August 2023, 6:35 pm

Mashabiki wa Simba tawi la Senga. Picha na Amon Bebe

Shamrashamra za kilele cha wiki ya Simba zimeendelea leo kufuatia wanachama Senga kuzindua tawi ikiwa ni muendelezo wa siku ya jana Simba Day.

Na Amon Bebe- Geita

Leo wanachama wa klabu ya Simba kijiji cha Chanika kata ya Senga, Mkoani Geita wamefanya sherehe ya uzinduzi wa tawi lao, ambapo mpaka sasa tawi hilo lina wanachama 150 na wametumia kiasi cha shilingi laki 7 kwaajili ya ujenzi wa mnara wa tawi hilo huku wakiwa na mpango wa ujenzi wa ofisi pamoja na ukumbi wa mikutano kwaajili ya matumizi yao.

Daniel Mafuru mwenyekiti pamoja na katibu wa tawi hilo wanazungumzia maendeleo ya tawi hilo.

Mwenyekiti tawi la Simba Senga
Katibu wa tawi Simba Senga
Mashabiki wa Simba tawi la Senga. Picha na Amon Bebe

Kwa upende wake mgeni rasimi katika hafla hiyo ambaye ni Afisa mtendaji kata ya Senga Bw.Mihali Iddy Nyalema amesema uongozi wa kata hiyo utatoa ushirikiano katika ujenzi wa ofisi ya tawi hilo.

Afisa mtendaji kata ya Senga

Nao baadhi ya mamia wa mashabiki wa simba waliojitokeza katika sherehe hiyo walikuwa na haya ya kusema

Mashabiki wa Simba tawi la Senga
Mashabiki wa Simba tawi la Senga. Picha na Amon Bebe

Aidha katika sherehe hiyo Bank ya NMB imefanya Shughuli ya usajili wa wanachama kupitia mfumo mpya wa Kadi ambapo wanachama zaidi ya 20 wamejiandikisha.