Storm FM

Buzi wakamatwa Geita

4 June 2021, 9:50 pm

Baadhi ya wafugaji wa Mifugo aina ya mbuzi  katika Mtaa wa Mpomvu  kata ya Mtakuja Halmashauri ya mji wa Geita  wamefika  nakutoa malalamiko katika ofisi  ya mtaa huo kutokana na mbuzi wao kukamatwa bila kufuata utaratibu unaotakiwa.

Wafugaji Mpomvu

Aidha wananchi wa eneo hilo wamesema kutokana na baadhi ya mifugo kuzagaa mitaani hali hiyo inasababisha uharibifu ikiwemo bidha sokoni na kuushauri uongozi wa eneo hilo kusimamia sheria ili kutataua changamoto hiyo.

Nae Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa huo  Bw Matiasi Metusela  ametumia fursa hiyo kuwataka  wafugaji  kuendelea kuzingatia kanuni na taratibu za ufugaji ili kuondokana nachangamoto ya mifugo kuzagaa mitaani.