Storm FM

Miundombinu ya usafiri Mkoani Geita yaboreshwa

29 March 2021, 5:14 pm

Watumiaji wa vyombo vya moto mkoa wa   Geita   wamesema hayati Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano watanzanaia Watamuuenzi  kwa vitendo  kwakuwa alisimamia na kuboresha Miundombinu ya usafiri.

Hayo yamesemwa na  Mwenyekiti wa umoja wa magari madogo Tax Mkoa wa Geita Bw Charles  Martin   wakati akizungumza na Storm Fm katika kituo cha magari hayo ambapo amebainisha namna ambavyo jitihada kubwa zilizofanywa na hayati magufuli kwakusimamia  vyema miundombinu ya usafiri.

Aidha watumiaji wa vyombo vya moto  mjini Geita  wamesema moja kati ya vitu ambavyo  viliigusa nafsi zao ni pamoja na kudhibiti wizi kwenye vyombo vya usafiri  hali ambayo imeleta amani kwa watanzania.

Hayati  Dkt John Pombe Magufuli alihakikisha anasimamia miundombinu ya vyombo vya usafiri kwa kuweka miundo mbinu safi ya barabara sambamba na madaraja kama ambvyo alieleza wakati yupo Jijini Mwanza kwenye uzinduzi wa Daraja la Furahisha.