Storm FM

Wananchi wachoshwa na ajali, waanzisha ujenzi wa shule Lumasa.

30 May 2024, 10:21 am

Muonekano wa jengo la shule shikizi inayojengwa kitongoji cha Lumasa. Picha na Evance Mlyakado

Licha ya serikali kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu katika maeneo mbalimbali nchini, bado baadhi ya vijiji vinakabiliwa na changamoto.

Na: Evance Mlyakado – Geita

Wakazi wa kijiji cha Ibondo kitongoji cha Lumasa kata ya Buseresere wilaya ya Chato mkoani Geita wamelazimika kuanza ujenzi wa shule shikizi katika eneo hilo kufuatia vifo vya watu 17 wakiwemo wanafunzi 7 waliofariki kwa ajali wakati wakivuka barabara kwenda shule ya msingi Ibondo huku wakiiomba serikali kuwasaidia ili wakamilishe ujenzi wa shule hiyo.

Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa shule hiyo afisa mtendaji wa kijiji hicho Benjamini Mtalebwa  amesema vifo hivyo 17 ni kuanzia mwaka 2018  hadi sasa hali ambayo imewalazimu wakazi wa kijiji hicho kuchangishana kila kaya elfu 6000 ili kuweza kufanikisha ujenzi wa shule hiyo na sasa licha ya shule hiyo kutokukamilika inawanafunzi 258 ambao kwa sasa wanasomea kwenye ofisi ya mwenyekiti wa kitongoji

Sauti ya afisa mtendaji

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Chato Mandia Kihiyo amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo huku akisema halmashauri hiyo ipo tayari kuwaunga mkono wananchi hao katika ukamilishaji wa ujenzi wa shule hiyo.

Sauti ya mkurugenzi

Mkuu wa wilaya ya Chato Said Nkumba amewapongeza wananchi hao kwa kuanzisha ujenzi wa shule hiyo ili kudhibiti ajali hizo huku akimuagiza mkurugenzi wa halmashauri kuhakikisha shule hiyo inakamilika pamoja na kuisajili ili iweze kutambulika.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Chato