Storm FM

Mwenyekiti wa Mtaa anusurika kipigo kutoka kwa wananchi Geita

5 April 2021, 5:27 pm

Mwenyekiti wa mtaa wa Tambukareli kata ya Kalangalala Wilayani Geita amenusurika kipigo kutoka kwa wananchi wa mtaa wa Bombambili kwa madai ya kutaka kusoma taarifa ambayo hawakuitaka isomwe mbele yao.

Hatua hiyo ya wananchi imetokana na madai ya kiongozi huyo kuingilia majukumu ya mtaa mwingine bila kushirikisha uongozi wa Kata na mtaa wa bombambili hali ambayo wamedai kutokutambua ujio wa kiongozi huyo kwenye mtaa wao, ambapo mwenyekiti huyo alikuwa na lengo la kujadili kuhamishwa kwa mtaa wa bombambili kupelekwa katika mtaa wake wa Tambukareli

Mwenyekiti wa CCM kata ya bombambili Majigajiga  Faida Idebelyang’omi Akatoa msimamo kwa niaba ya wananchi wa mtaa wa Bomba mbili kutokukubaliana na maamuzi ya kuhamishwa mtaa wao kupelekwa mtaa wa Tambukareli, Kutokana na hali hiyo wakashindwa kufikia makubaliano hali iliyomlazimu mwenyekiti wa mtaa wa bombambili kufunga mkutano.