kkk
Storm FM

Familia zaidi ya 20 zaathiriwa na mafuriko Geita

8 April 2024, 9:13 pm

Hiki ni mojawapo kati ya vyoo vilivyozingirwa na maji kutokana na mafuriko yaliyoukumba mtaa wa Mbugani mjini Geita. Picha na Evance Mlyakado

Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Geita na nchi nzima kwa ujumla, athari mbalimbali zimeendelea kujitokeza kwa wananchi ikiwemo kuharibika kwa miundombinu ya barabara na athari nyinginezo katika mazingira.

Na Evance Mlyakado – Geita

Mvua kubwa iliyonyesha siku ya Jumapili katika maeneo mbalimbali ya mji wa Geita, imeziacha familia zaidi ya 20 zilizopo mtaa wa Mbugani kata ya Kalangalala, halmashauri ya mji wa Geita katika hali ya sintofahamu kutokana na makazi yao kuvamiwa na maji.

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa mbugani wakivuka maji. Picha na Evance Mlyakado

Wakizungumza na Storm fm wananchi hao wamesema kuwa maji  hayo yamezingira makazi yao baada ya mtaro unaopitisha maji kutoka katika daraja lililopo barabara kuu ya lami kupasuka na maji kusambaa katika makazi yao hali iliyosababisha wengi wao kushindwa kupika na kupata sehemu ya kujihifadhi.

Sauti za wananchi walioathiriwa wa mafuriko kutoka mtaa wa Mbugani, Geita.

Kwa upande wake meneja wa TARURA wilaya ya Geita, Mhandisi Bahati Subeya amesema kuwa shughuli za kiuchumi zinazoendeshwa kandokando ya mtaro huo na wananchi wa maeneo hayo ndio zimesababisha mtaro huo kupasuka na maji yake kuvamia makazi hayo licha ya onyo na makatazo kadhaa kutolewa na serikali.

Sauti ya meneja TARURA wilaya ya Geita
Hapa ni ndani ya nyumba ya mmoja kati ya wananchi walioathiriwa na mafuriko hayo. Picha na Evance Mlyakado