Storm FM

Wazazi wasiolea watoto kukiona cha moto Geita

16 April 2025, 3:00 pm

Kamanda wa Polisi akizungumza na wakazi wa katoro Geita kuhusu suala la ulinzi wa mtoto. Picha na Mrisho Sadick

Jeshi la polisi katika mkakati wa kukabiliana na changamoto ya vitedo vya ukatili kwa watoto Mkoani Geita

Na Mrisho Sadick:

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limeanza oparesheni ya kuwakamata watoto wanaozurura mitaani nyakati za usiku na kuwawajibisha wazazi wao ili kukabiliana na changamoto ya vitendo vya ukatili ikiwemo vya ulawiti  kwa watoto hao. 

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Geita kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Safia Jongo wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Katoro wilayani Geita ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Elimu ya Polisi Jamii inayofadhiliwa na Mgodi wa GGML.

Sauti kamanda wa polisi Geita
Maafisa wa jeshi la polisi ,viongozi na wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara. Picha na Mrisho Sadick

Kwa upande wake mrakibu msaidizi wa jeshi la polisi kutoka makao makuu dawati la jinsia na ulinzi wa mtoto Wilfred Willa amewataka wazazi na walezi kuwajibika kwa watoto ikiwemo kujenga utamaduni wa kuwakagua watoto hao mara kwa mara.

Sauti ya mrakibi msaidizi wa polisi Willa

Baadhi ya wakazi wa Kata hiyo wamepongeza hatua ya Jeshi la Polisi kuanzisha oparesheni hiyo itakayo kuwa msaada kwa watoto hao huku wakiwaomba wazazi kuhakikisha wanawajibika kwa watoto wao ili kukabiliana na changamoto ya vitendo vya ukatili kwa watoto.

Sauti ya wananchi Katoro