Storm FM

Aliyevamia mkondo wa maji kikaangoni Geita

15 July 2026, 1:52 pm

Vifusi vilivyomwagwa katika mkondo wa maji. Picha na Kale Chongela

Hatua hiyo inaweza kusababisha kuziba kwa njia ya maji na kuongeza hatari ya mafuriko wakati wa mvua, jambo ambalo linaweza kuathiri makazi ya wananchi wanaozunguka eneo hilo.

Na: Kale Chongela

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, Malezi na Mazingira chama  cha mapinduzu CCM  katika Mtaa wa 14 Kambarage,  Kata ya Buhalahala Manispaa ya Geita ameiomba serikali ya mtaa huo kuchukua hatua dhidi ya Bw. Yuga Mabiza Ndoto anayedaiwa kumwaga vifusi katika Bode lililoachwa wazi na wananchi ukwa ajili ya kupitisha maji ya mvua

Akizungumza na Storm Fm Mwenyekiti huyo Bw Omary Seifu  amesema hatua hiyo inaweza kusababisha kuziba kwa njia ya maji na kuongeza hatari ya mafuriko wakati wa mvua, jambo ambalo linaweza kuathiri makazi ya wananchi wanaozunguka eneo hilo.

Sauti ya mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, Malezi na Mazingira CCM Mtaa wa 14 Kambarage

Kwa upande wake anayedaiwa kuvamia katika njia hiyo Bw Yuge Mabiza ndoto ameiambia Storm Fm kuwa eneo hilo analimiki zaidi ya miaka 20 na kwamba matarajio yake baada ya kujaza vifusi hivyo atajenga mtaro kwa lengo la kupitisha maji ya mvua.

Sauti ya anayedaiwa kuvamia katika njia ya maji Bw Yuge Mabiza

Mwananchi akipita katika mkondo wa maji. Picha na Kale Chongela

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa 14 kambarage Bw James Sanyege amekiri kuwepo hali hali hiyo na kuahidi kuwa zoezi la utatuzi limeshaanza ikiwemo kumuandikia barua la kustisha uweka wa vifusi katika eneo hilo .

Sauti ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa 14 kambarage