

15 April 2025, 1:42 pm
Madereva wa vyombo vya usafiri vya kibiashara mkoani Geita wamekutaka kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ya usajili LATRA
Na Mrisho Sadick:
Kufuatia mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kuwataka madereva wa vyombo vya moto vya kibiashara na watoa huduma kwenye vyombo hivyo nchini kusajiliwa, baadhi ya madereva mkoani Geita wamepokea suala hilo kwa mikono miwili huku wakiiomba serikali kutoa elimu kwanza kabla ya kuanza kuwachukulia hatua.
Wakiwa kwenye kikao kilichowakutanisha madereva wa magari ya abiria na viongozi wa umoja huo kutoka wilaya zote za mkoa wa Geita katika manispaa ya Geita kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili ambapo wamegusia suala la watoa huduma kupatiwa mafunzo na usajali wa madereva.
Mwenyekiti wa umoja wa wasafirishaji mkoa wa Geita Ismail Ibrahim ameiomba serikali kusogeza huduma ya mafunzo hapo Geita nakutoa elimu kwa madereva na watoa huduma kabla ya kuanza kuchukua hatua.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Geita Lazaro Masembo mbali nakuahidi kushughulikia changamoto zote zilizotolewa na madereva hao amewataka kuchukua tahadhari kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha ili kuepukana na ajali.