Storm FM

Wamiliki wa Karasha na Mwalo wabanwa kujenga Vyoo

19 August 2026, 2:12 pm

Picha ya muonekano wa mwalo katika eneo la Kumbayaga. Picha na Kale Chongela

Uwepo wa vyoo ni muhimu katika kulinda usafi wa mazingira na afya za watu wanaojihusisha na shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini.

Na: Kale Chongela

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Ndugu Yefred Myenzi, amewataka wamiliki wa maeneo ya uchimbaji na uchenjuaji wa madini ya dhahabu, ikiwemo mwalo na karasha, kuhakikisha wanaweka huduma za vyoo katika maeneo yao ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira.

Myenzi ameyasema hayo wakati akizungumza na Storm FM, ambapo amesisitiza kuwa uwepo wa vyoo ni muhimu katika kulinda usafi wa mazingira na afya za watu wanaojihusisha na shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita

Amesema baadhi ya maeneo yanayotumika kwa shughuli hizo yanaweza kuwa chanzo cha uchafuzi wa mazingira endapo wachimbaji na wafanyakazi hawatapata huduma bora za vyoo.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita

Aidha, amewataka wamiliki wa maeneo hayo kuzingatia usafi wa mazingira na kuhakikisha wanatoa huduma muhimu kwa watu wanaofanya shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini, kwa lengo la kulinda afya za jamii na mazingira kwa ujumla.

Moja ya pori ambalo wachimbaji hutumia kama sehemu ya kujisaidia. Picha na Kale Chongela