Storm FM

Madereva wa mabasi Geita walalamikia mfumo wa ukatwaji pointi kwenye leseni

15 September 2026, 4:50 pm

Baadhi ya madereva wa magari ya abiria mkoani Geita. Picha na Kale Chongela

Uwepo wa pointi lukuki imeendelea kuathiri kazi ya udereva huku ukiomba kuwepo kwa utaratibu wa haki na uwazi katika utekelezaji wa sheria za usafirishaji.

Na: Kale Chongela

Madereva wa magari ya abiria mkoani Geita wameiomba serikali kuangalia upya sheria ya kukata pointi kwenye leseni za madereva pindi wanapokutwa na makosa wakiwa barabarani jambo ambalo linasababisha msongo wa mawazo kwa madereva na kupelekea ajali za mara kwa mara.

Madereva hao wamewasilisha kero hiyo katika ofisini ya umoja wa madereva Tanzania (UWAMATA) wakieleza uwepo wa pointi nyingi za makosa ya barabarani pamoja na ufungaji wa leseni za udereva imekuwa ikiathiri shughuli zao za usafirishaji.

Sauti ya madereva wa magari ya abiria

Katibu wa umoja wa madereva Mkoa wa Geita Bw Baraka Henry Cosmas ametumia fursa hiyo kuiomba  Serikali kupitia mamlaka husika kusikiliza changamoto zao na kutoa elimu zaidi kuhusu matumizi ya mfumo huo

Sauti ya katibu wa umoja wa madereva Mkoa wa Geita

Makamu Mwenyekiti  wa umoja wa madereva Tanzania (UWAMATA) Bw Ismail Ibrahimu  amesema uwepo wa pointi lukuki imeendelea kuathiri kazi ya udereva huku ukiomba kuwepo kwa utaratibu wa haki na uwazi katika utekelezaji wa sheria za usafirishaji.

Sauti ya makamu Mwenyekiti  wa umoja wa madereva Tanzania

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Geita Kamishna Msaidizi wa Polisi Mathayo Msuyale amesema kuwa uwepo wa kanuni za usalama barabarani unalenga kuhakikisha madereva wanazingatia sheria na kupunguza ajali za barabarani.

Sauti ya mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Geita

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Geita Kamishna Msaidizi wa Polisi Mathayo Msuyale. Picha na Kale Chongela