Storm FM

Polisi Jamii Run Club yazinduliwa Geita ili kuimarisha mahusiano na Jamii

22 August 2026, 1:07 pm

Baadhi ya washiriki wa Polisi Jamii run club wakiwa na bango lenye kaulimbiu isemayo “Tushirikiane kuimarisha amani, usalama na umoja wa kitaifa”. Picha na Ester Mabula

Polisi Jamii ilianzishwa Agosti 25, 2006 na IGP Mstaafu Said Mwema kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na Jamii ambapo maadhimisho hayo yameenda sambamba na zoezi la uchangiaji wa damu wa hiari.

Na: Ester Mabula

Jeshi la polisi mkoa wa Geita leo Agosti 22, 2026 limeadhimisha miaka 20 ya kuanzishwa kwa Polisi jamii nchini kwa kuzindua Polisi Jamii Run Club yenye lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya na Jeshi la polisi na wananchi kupitia michezo mbalimbali.

Akizungumza wakati wa maadhimsiho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kalangalala Manispaa ya Geita, Kamanda wa polisi mkoa wa Geita SACP Safia Jongo amesema dhana ya polisi Jamii imeendelea kuacha alama ya umoja na ushirikiano baina ya Jeshi la polisi na wananchi.

Sauti ya Kamanda Geita SACP Safia Jongo
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita SACP Safia Jongo akizungumza katika maadhimisho hayo. Picha na Ester Mabula

Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Geita amesema ushirikiano baina ya Jeshi la polisi na wananchi ni muhimu kwani unaendelea kusaidia kuimarisha mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu nchini huku akilipongeza Jeshi la polisi mkoa wa Geita kwa maadhimisho hayo.

Sauti ya mgeni rasmi, RC Geita Martine Shigela
Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela akizungumza katika maadhimisho hayo. Picha na Ester Mabula

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Amina Kahando ambaye ni mkuu wa Polisi Jamii mkoa wa Geita amesema maadhimisho hayo yamehususha washiriki kutoka maeneo mbalimbali huku baadhi ya washiriki wakieleza umuhimu wa kushiriki katika maadhimisho hayo.

Sauti ya ACP Amina Kahando na baadhi ya washiriki
Baadhi ya washiriki ambao ni Polisi Jamii fitness Centre kutoka wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. Picha na Ester Mabula