Storm FM
Storm FM
2 October 2026, 5:05 pm

Serikali kupitia wizara ya madini nchini imeendelea kusimamia utekelezaji wa sheria ya ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini (local content) ambayo inalenga kuwawezesha wazawa kunufaika kupitia shughuli za madini.
Na: Ester Mabula
Kupitia kongamano lililofanyika leo Oktoba 03, 2026 lililoandaliwa na Tume ya madini nchini likihusisha wananchi, wadau wa madini pamoja na viongozi mbalimbali mkoani Geita, Mwenyekiti wa tume hiyo Dkt. Janeth Lekashingo amesema lengo kuu la sheria hiyo ni kuwezesha ushiriki wa makampuni ya kitanzania kufanya kazi kwa ushindani na kufikia malengo ambapo Tume ya madini itaendelea kusimamia sheria hiyo kikamilifu ili kufikia azma hii.

Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mhandisi Chacha Wambura amewahimiza wana Geita kuchangamkia fursa kupitia sheria hiyo huku Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Alexander Mnyeti akipongeza uwepo wa sheria hiyo na kutoa rai kwa watanzania kuacha uvivu na kufanya kazi kwa ushindani ili kuitekeleza vyema sheria hiyo.
Mgeni rasmi, Waziri wa madini Mhe. Anthony Mavunde amesema kwa mwaka migodi hutumia Tsh. Trilioni 5.1 kwaajili ya manunuzi ya bidhaa na huduma na kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha asilimia 90 ya fedha hiyo inawanufaisha watanzania.
