Storm FM

Geita yawaka taa 400 za barabarani usalama waimarishwa

9 October 2026, 2:08 pm

Muonekano barabarani wakati wa usiku taa zikiwa zinamulika. Picha na Ashura Ramadhani

Taa hizo ni muhimu hasa katika kipindi cha mvua, kwa kuwa zinasaidia madereva kuona vizuri na kuongeza usalama kwenye barabara yenye matumizi makubwa ya magari.

Na: Ashura Ramadhani

Tahadhari juu ya Mvua za El-Nino Katika Mkoa wa Geita Taa 400 za barabarani zimefungwa kuanzia Mwatolole hadi Nyankumbu na maeneo mengi lengo likiwa ni kuimarisha usalama wa madereva na wananchi nyakati za usiku.

Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Geita, Mhandisi Hosea Machaka, amesema uwekaji wa taa hizo ni muhimu hasa katika kipindi cha mvua, kwa kuwa zinasaidia madereva kuona vizuri na kuongeza usalama kwenye barabara yenye matumizi makubwa ya magari.

Sauti ya kaimu meneja wa TANROADS mkoa wa Geita

Mhandisi Machaka amewataka wananchi kushirikiana na Serikali kulinda na kutunza miundombinu hiyo ili iendelee kutoa huduma na kuchangia usalama pamoja na maendeleo ya kiuchumi.

Nao wafanyabiashara Mkoa Geita wamesema taa hizo zimebadili mazingira ya biashara maeneo yao kwa kuongeza muda wa kufanya biashara tofauti na mwanzo ambapo walilazimika kufunga biashara mapema kutokana na giza.

Sauti ya wafanyabiashara

Mmoja wa wafanyabiashara wa matikiti akiwa anafanya kazi wakati wa usiku. Picha na Ashura Ramadhani