Storm FM

Redio jamii kanda ya ziwa zatakiwa kuwapa nafasi watu wenye ulemavu

19 October 2026, 10:52 am

Washiriki wa mafunzo ma wakufunzi wakiwa katika picha ya pamoja. Picha na Recho David

Mafunzo hayo yanatarajiwa kusaidia kubadili namna wanahabari wanavyoibua na kuripoti masuala ya watu wenye ulemavu, huku yakichochea ushiriki wenye maana wa kundi hilo katika vipindi mbalimbali vya redio.

Mrisho Sadick:

Waandishi wa habari kutoka redio 14 za jamii Kanda ya Ziwa wametakiwa kuongeza taarifa zinazohusu watu wenye ulemavu na kuhakikisha wanashirikishwa kikamilifu katika vipindi vya redio ili kukuza usawa, kupunguza unyanyapaa na kuimarisha uwakilishi wao katika jamii.

Wito huo umetolewa na  Mhariri wa Jukwaa hilo Hilali Ruhundwa katika mafunzo yaliyoandaliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Vyombo vya Habari Finland (VIKES) kwa ufadhili wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland kwa lengo la kuimarisha uwezo wa wanahabari katika kuibua changamoto, mafanikio na mahitaji ya watu wenye ulemavu nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) takribani watu bilioni 1.3 duniani sawa na asilimia 16 ya idadi ya watu wote wanaishi na ulemavu mkubwa takwimu hizi zinaonesha umuhimu wa kuhakikisha kundi hilo linapata fursa sawa za kushiriki katika maisha ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Mkufunzi Amua Rushita akiwa katika mafunzo na washiriki. Picha na Mrisho Sadick

 amesema redio za jamii zina nafasi ya kipekee katika kufikisha taarifa kwa wananchi na kuibua masuala yanayowagusa watu wenye ulemavu kutokana na ukaribu wake na jamii huku akiongeza kuwa mafunzo hayo yanatarajiwa kusaidia kubadili namna wanahabari wanavyoibua na kuripoti masuala ya watu wenye ulemavu, huku yakichochea ushiriki wenye maana wa kundi hilo katika vipindi mbalimbali vya redio.

Kwa upande wake Tuma Dandi miongoni mwa wakufunzi wa mafunzo hayo amesema kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 tanzania inakadiriwa kuwa na idadi ya watu wenye ulemavu zaidi ya milioni 6 nakwamba vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kuelimisha jamii na kubadili mitazamo hasi dhidi ya watu wenye ulemavu.

Sambamba na hilo Dandi ameiomba serikali kuzingatia umuhimu wa kutoa ruzuku au msaada wa kijamii kwa watu wenye ulemavu mkali wanaokabiliwa na changamoto za kiuchumi ili kuwawezesha kupata mahitaji muhimu na kuishi kwa utu.

Mhariri wa Jukwa la Radio Portal Hilal Ruhundwa akiwa katika mafunzo. Picha na Mrisho Sadick

Naye mkufunzi Amua Rushita amesisitiza kuwa redio za jamii zinapaswa kuwashirikisha moja kwa moja watu wenye ulemavu katika vipindi mbalimbali badala ya kuzungumza kuhusu maisha yao bila kuwapa nafasi ya kueleza uzoefu maoni na mahitaji yao.

Baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo wamekiri kuwa imani potofu kuhusu watu wenye ulemavu bado zipo katika jamii. Wamesema wamepata uelewa utakaowasaidia kuboresha uandishi wao, kupinga ubaguzi na kutoa nafasi sawa kwa watu wenye ulemavu katika vipindi na taarifa wanazozalisha.

Ripoti ya Stori hii na Mrisho Sadick