Storm FM

Wanafunzi, wazazi na watoa tiba asili waelimishwa mapambano ya selimundu

29 September 2026, 2:19 pm

Mkurugenzi wa shirika la Tanzania Sickle cell warriors organization Bi. Pacskazia Thomas Mazeze akizungumza na washiriki (hawapo pichani). Picha na Ester Mabula

Mwezi Septemba ni mwezi wa uelewa juu ya ugonjwa wa sicle cell duniani ambapo mataifa hufanya shughuli mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu kwa jamii juu ya ugonjwa huo ambapo kwa mkoa wa Geita kilele cha maadhimisho kimefanyika leo Septemba 29, 2026.

Na: Ester Mabula

Jamii imekumbushwa kupima ugonjwa wa selimundu (sickle cell) ili kuweza kubaini hali zao na kusaidia kuepuka kupata watoto wenye viashiria na vinasaba vya ugonjwa huo.

Hayo yameelezwa leo Septemba 29, 2026 na Mkurugenzi wa shirika la Tanzania Sickle cell warriors organization Bi. Pacskazia Thomas Mazeze wakati akizungumza na wanafunzi, wazazi/walezi na watoa huduma za tiba asili katika ukumbi wa mikutano EPZA  ambapo amesema shirika hilo linaendelea kutoa elimu kwa jamii ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo.

Sauti ya Bi. Pacskazia Thomas Mazeze
Mwanafunzi akiwa na bango lenye ujumbe wa mapambano ya ugonjwa wa selimundu. Picha na Ester Mabula

Mratibu wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza mkoa wa Geita Dkt. Glory Temba amesema kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari 2026 hadi Julai 2026 wamefanya upimaji wa watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano ambapo watoto 209 walikutwa na vinasaba vya ugonjwa huo kati ya watoto 6858 waliofanyiwa vipimo.

Sauti ya Dkt. Glory Temba
Mratibu wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza mkoa wa Geita Dkt. Glory Temba akizungumza na washiriki (hawapo pichani). Picha na Ester Mabula

Wakizungumza baada ya kupata elimu, baadhi ya washiriki wamepongeza uwepo wa elimu hiyo na kueleza kuwa itasaidia kuendelea kujenga uelewa zaidi kwa jamii na kuachana na imani potofu juu ya ugonjwa huo.

Wanafunzi wa shule ya sekondari Bombambili wakipewa elimu ya selimundu iliyofanyika leo. Picha na Ester Mabula