Storm FM

Wafugaji kata ya Shiloleli wapatiwa dawa za kuogesha mifugo

13 August 2026, 4:22 pm

Baadhi ya wafugaji na wachungaji wa mifugo wakiwa katika zizi la ng’ombe katika kata ya Shiloleli. Picha na mwandishi wetu

Kata ya Shiloleli inapatikana katika halmshauri ya manispaa ya Geita ambapo inakadiriwa kuwa na jumla ya Ng’ombe 3647, Mbuzi 1420 na Kondoo zaidi ya 900.

Na: Ester Mabula

Wafugaji wa kata ya Shiloleli, halmashauri ya manispaa ya Geita, wameanza kunufaika na dawa za kuogeshea mifugo zenye thamani ya Sh milioni 1.5 zilizotolewa na Mbunge wa Geita Mjini, Mhandisi Chacha Wambura, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyotoa kwa wananchi wa eneo hilo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Afisa Mifugo wa Kata ya Shiloleli, kwa niaba ya wananchi, kumuomba Mbunge Wambura kusaidia upatikanaji wa dawa za kuogeshea mifugo katika josho lililopo katika eneo hilo.

Baadhi ya mifugo aina ya ng’ombe katika zizi linalolopatikana eneo la Shiloleli. Picha na Mwandishi wetu

Akijibu ombi hilo, Mhandisi Chacha Wambura aliahidi kuhakikisha kuwa ndani ya kipindi cha miezi sita anagharamia upatikanaji wa dawa hizo, ili kuwawezesha wafugaji kuendelea na huduma ya uogeshaji wa mifugo bila kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa dawa.

Sauti ya mbunge, Chacha Wambura

Akizungumza kuhusu umuhimu wa zoezi hilo, Daktari wa Mifugo wa Manispaa ya Geita Jeremia Njile amesema uogeshaji wa mifugo ni muhimu katika kudhibiti wadudu wanaosababisha magonjwa mbalimbali kwa mifugo.

Sauti ya daktari wa mifugo
Daktari wa mifugo Jeremia Njile akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Picha na mwanandishi wetu

Mwenyekiti wa eneo hilo na baadhi ya wafugaji wamesema msaada huo umewawezesha kupata dawa zinazotumika katika kuogesha mifugo mbalimbali, ikiwemo ng’ombe, mbuzi na kondoo, hatua ambayo itasaidia kudhibiti wadudu na magonjwa yanayoweza kuathiri afya ya mifugo.

Sauti ya mwenyekiti na wananchi