Mazingira FM

Wazazi watakiwa kuzingatia usafi na ulinzi wa watoto

1 October 2026, 10:24 pm

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Bunda, Marysiana Sabuni

UWT ni nguzo muhimu ya CCM, hivyo wanawake wanapaswa kutumia nafasi yao kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya mazingira hatarishi.

Na Adelinus Banenwa

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Bunda, Marysiana Sabuni, amewataka wanawake kuzingatia usafi wa mazingira pamoja na kushiriki kikamilifu katika ulinzi na malezi ya watoto.

Marysiana ametoa wito huo wakati wa kilele cha maadhimisho ya UWT wilayani Bunda, ambapo jumuiya hiyo imehitimisha maadhimisho hayo kwa kufanya usafi katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bunda.

Amesema, pamoja na kufanya shughuli mbalimbali za kijamii katika ngazi za matawi na kata wakati wa maadhimisho hayo, wameamua kuhitimisha kwa kufanya usafi katika ofisi za chama kama sehemu ya kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa usafi wa mazingira.

Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bunda.

Marysiana amesema UWT ni nguzo muhimu ya CCM, hivyo wanawake wanapaswa kutumia nafasi yao kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya mazingira hatarishi.

Sauti ya Marysiana Sabuni

Elizabert Jonathan kaimu katibu wa UWT Bunda amesema usafi unaofanywa unalengo la kudumisha hali ya usafi katika jamii ameongeza kuwa sambamba na usafi huo bado anaendelea kutoa wito kwa jamii kujiandaa na athari zinazoweza kutokana na mvua za el-nino kama ambavyo ilivyotabiliwa

Sauti ya Elizabert Jonathan kaimu katibu wa UWT Bunda