Mazingira FM
Mazingira FM
12 April 2026, 8:19 am

Watumishi wa TRA kuwahudumia wafanyabiashara kwa haki na uwazi, pamoja na kuwafuata katika maeneo yao ya biashara ili kufanya makadirio sahihi.
Na Adelinus Banenwa
Wafanyabiashara wote nchini wametakiwa kuwasilisha malalamiko iwapo wanahisi wamekadiriwa kodi zaidi au pungufu ya kipato chao ili kufanyiwa tathmini upya.
Ujumbe huo umetolewa leo Aprili 14, 2026 na Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Juma Mwenda, wakati wa mkutano wake na wafanyabiashara wilayani Bunda, mkoani Mara.
Amesema TRA itaendelea kuwasikiliza walipakodi kila Alhamisi pamoja na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji kodi ikiwemo IDRAS. Aidha, amewataka wafanyabiashara kuepuka vitendo vya rushwa huku akisisitiza vita ya dhidi ya wakwepa kodi inaendelea.

Kwa upande wao, wafanyabiashara wamependekeza kuboreshwa kwa mashine ndogo za EFD, kupunguzwa kwa VAT kutoka asilimia 18 , pamoja na kuzingatia uwiano wa faini na thamani ya mzigo uliokamatwa.

Naye Kamishna wa Kodi za Ndani, Michael Muhoja, amewataka watumishi wa TRA kuwahudumia wafanyabiashara kwa haki na uwazi, pamoja na kuwafuata katika maeneo yao ya biashara ili kufanya makadirio sahihi.