Mazingira FM
Mazingira FM
30 April 2026, 1:31 pm

Kitendo cha kamati kuu kumteua ndugu Kambarage katika watu 6 ni jambo la heshima na hii inaonesha bado Bunda inaaminika.
Na Adelinus Banenwa
Chama cha mapinduzi wilaya ya Bunda kimesema kimepokea kwa furaha uwamuzi wa kamati kuu ya CCM taifa kumpendekeza Ndugu Kambarage Masatu Wasira kuwania afasi ya ubunge wa Afrika Mashariki.
Gasper Petro Charles katibu wa siasa uenezi na mafunzo chama cha mapinduzi wilaya ya Bunda Akizungumza na radio mazingira fm amesema kitendo cha kamati kuu kumteua ndugu Kambarage katika watu 6 ni jambo la heshima na hii inaonesha bado Bunda inaaminika.

Ndugu Gasper amesema mbali na kamati kuu kumpendekeza ndugu Kambarage pia kwa wilaya ya Bunda ni kiongozi wa kamati ndogo ya uchumi fedha na mipango CCM wilaya ya Bunda pia amewahi kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa pia alikuwa mtia nia ubunge jimbo la Bunda mjini uchaguzi wa 2025.
Ikumbukwe wateule wote sita kwa upande wa wanaume na watatu kwa upande wa wanawake watapigiwa kura leo April 30 na wabunge wa chama cha mapinduzi na kupata majina mawili upande wa wanaume na jina moja la mwanamke miongoni mwa wateule hao kabla ya kithibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makada wengine walioteuliwa na Kamati Kuu ya Halmashauri ya CCM katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam jana, ni Stephen Lujwahuka Byabato, Cosato David Chumi, Jabir Jafar Bwanika, Paschal Lawrence Masalu na Suleiman Hassan Serera.
Aidha, Kamati Kuu hiyo iliwateuwa wanawake watatu – Chikulupi Njelu Kasaka, Fatuma Abdallah Kange na Jesca Julias Mshama kuwania nafasi moja katika Bunge la Afrika Mashariki.