Mazingira FM

Mwili uliozikwa kwa kukosa ndugu Bunda wafukuliwa baada ya ndugu kupatikana

29 January 2024, 2:38 pm

Sehemu ambayo mwili wa mwanamke ambao aliyeokotwa umezikwa, Picha na Adelinus Banenwa

Mwili wa mwanamke uliozikwa kwa kukosa ndugu eneo la mtaa wa Tamua kata ya Nyatwali halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara umefukuliwa baada ya wanaodaiwa kuwa ndugu kupatikana.

Na Adelinus Banenwa

Mwili wa mwanamke uliozikwa kwa kukosa ndugu eneo la mtaa wa Tamua kata ya Nyatwali halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara umefukuliwa baada ya wanaodaiwa kuwa ndugu yao kupatikana.

Mwili huo uligundulika mnamo januari 9, 2024 katika mwambao wa ziwa Victoria eneo la mtaa wa Tamau ujaruoni  ambapo baada ya taratibu za jeshi la polisi na wananchi kushindwa kumtambua jeshi hilo lililoruhusu uzikwe na wananchi wa mtaa huo.

Mwenyekiti wa mtaa wa Tamau ndugu Asafu Elenesti Owiti ameiambia Mazinguira Fm wakati wa  zoezi la kufukua mwili huo kuwa, baada ya kutio hilo kuripotiwa na Redio Mazingira Fm alipokea simu ya wito kutoka polisi ili kutambua wanaodaiwa kuwa ndugu wa marehemu huyo.

Kwa upande wake Rose Muhoja anayetajwa kuwa mama mkubwa wa marehemu amesema mtoto wao anatambulika kwa jina la Ratifa Msafiri Mangu mwenye umri wa miaka 28 ambapo wamehakikisha kama familia kuwa yule aliyezikwa Tamau ni binti yao baada ya maelezo ya wananchi wa Tamau pia baada ya kuona picha waliooneshwa .