Mazingira FM

Sekondari ya Nyiendo kuwekewa umeme vyumba sita vya madarasa

14 October 2023, 1:28 pm

Eng  Kambarage Wasira mgeni rasmi katika mahafali Yya shule ya sekondari Nyiendo, Picha na Edward Lucas

Eng. Kambarage Wasira kwa kushirikiana na mdau wa maendeleo ndugu Eng.Gasper Mchanga wameahidi kuweka umeme katika madarasa 6 shule ya Sekondari Nyiendo iliyopo Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoani Mara.

Na Adelinus Banenwa

Mfumo wa umeme utakaogharimu shilingi milioni mbili  laki moja na sabini na sita elfu (2,176,000) unatarajiwa kufugwa katika vyumba 6 vya madarasa shule ya Sekondari Nyiendo iliyopo kata ya Kabarimu halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara.

Akizungumza katika mahafali ya 16 ya wanafunzi wa kidato Cha nne  Eng  Kambarage Wasira mgeni rasmi katika mahafali hiyo amesema pamoja na kuwepo kwa changamoto nyingi shuleni hapo lakini suala la kuwepo kwa nishati ya umeme katika madarasa kutawawezesha wanafunzi kujifunza kwa uhuru hasa wanaowahi kufika shuleni asubuhi na wale wanaochelewa kutoka hasa madarasa ya mitihani.

Kambarage amesema kwa kushirikiana na mdau wa maendeleo ndugu Eng.Gasper Mchanga wataweka umeme katika madarasa 6 ya shule hiyo ili iwe rahisi kwa wanafunzi kujisomea.

Aidha amewapongeza wazazi kwa kuhamasisha wanafunzi kwenda shule huku akiangazia idadi ya wanafunzi walioanza shule na wale walihitimu leo ikiwa ni tofauti ya wanafunzi watano tu.

Mkuu wa shule ya sekondari Nyiendo madam Merida Maeda Picha na Adelinus Banenwa

Kupitia taarifa ya shule iliyosomwa na mkuu wa shule hiyo Merida Maeda mbele ya mgeni rasmi amesema changamoto kubwa shuleni hapo ni suala la umeme kwenye madarasa jambo linalosababisha wanafunzi wanaowahi shuleni asubuhi kushindwa kujisomea kutokana na kukosa mwanga pia changamoto ya ushirikiano kati ya wazazi na uongozi wa shule akibainisha wazazi kushindwa kuchangia chakula Cha watoto shuleni

Changamoto zingine ni matundu ya vyoo, matenk ya kuvunia maji ya mvua na maabala mbili pamoja na maktaba.

Sauti ya mkuu wa shule Merida Maeda akibaindisha changamoto
Wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Nyiendo Picha na Edward Lucas

Awali wakisoma  risala mbele ya mgeni Rasmi wanafunzi wa kidato Cha nne wamesema mwaka 2020 walianza shule wakiwa 185 kati yao wavulana 93 na wasichana 92 ambapo hadi wanahitimu wamebaki wanafunzi 180 na kufanya idadi ndogo ya wanafunzi ambao hawajamaliza shule.

risala ya wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Nyiendo