Mazingira FM

Wanafunzi 4953 kidato cha nne Bunda kuanza mtihani Nov 13

12 November 2023, 7:43 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Naano wakati akifanya mahojiano na radio Mazingira Fm Picha na Thomas Masalu

Wanafunzi wapatao 4953 kidato cha nne wanatarajia kuanza mtihani wa kuhitimu kidato cha nne wilayani Bunda kati yao wasichana ni 2470 na wavulana 2483.

Na Adelinus Banenwa

Wanafunzi wapatao 4953 kidato cha nne wanatarajia kuanza mtihani wa kuhitimu kidato cha nne wilayani Bunda kati yao wasichana ni 2470 na wavulana 2483.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Naano wakati akifanya mahojiano na radio Mazingira Fm.

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Naano wakati akifanya mahojiano na radio Mazingira Fm Picha na Thomas Masalu

Mhe Naano amesema hadi sasa maadandalizi ya mitihani hiyo yamekamilika ikiwa ni pamoja na semina elekezi kwa wasimamizi wa mitihani na usambazaji wa mitihani katika maeneo husika miongoni.

mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Naano

Aidha Mhe Dkt Naano ameonya kwa wazazi na walezi, walimu pamoja na wanafunzi wenyewe juu ya kujihusisha na aina yoyote ya wizi na udanganyifu katika mitihani hii kuwa hwatosita kuwachukulia hatua watakaobainika.

mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Naano

Ikumbukwe kwamba kwa mujibu wa baraza la mitihani Tanzania NECTA mitihani ya kuhitimu kidato cha nne itaanza tarehe 13 November 2023, na utatamatika tarehe 30 november 2023.