Mazingira FM

Vijana wa kanisa la Baptist Nyasura wawatembelea wagonjwa hospital ya Bunda DDH

22 September 2023, 3:34 pm

Baadhi ya vijana kutoka kanisa la Baptist waliofika Hospitali ya Bunda DDH, Picha na Adelinus Banenwa

Umoja wa vijana kutoka kanisa la Nyasura Baptist Wakiongozwa na mchungaji wao kiongozi Jeremiah Motomoto wamefanya ziara ya kuwatembelea wagonjwa hospital ya Bunda DDH Kwa lengo la kuwatia moyo na kuwaombea

Na Adelinus Banenwa.

Akizungumza katika ziara hiyo Gratina Goshogi Dadi Kwa niaba ya vijana wengine amesema wameamua kuwatembelea wagonjwa Kwa kizingatia Imani yao inawaelekeza kuwatembelea wagonjwa na watu wasiyojiweza

Aidha amewataka vijana na watu wote wenye uwezo wa afya njema waweze kufika hospitali kuwasalimia na kuwatia moyo wagonjwa maana hiyo ndiyo furaha yao.

Mchungaji kiongozi wa kanisa la Baptist Nyasura Jeremiah Motomoto.Picha Adelinus Banenwa

Kwa upande wake mchungaji kiongozi wa kanisa la Baptist Nyasura Jeremiah Motomoto amesema lengo la kufika hospital Bunda DDH ni kuwaombea na kuwapa pole wagonjwa wote wanaondelea kupata matibabu kulingana na maagizo ya Imani yao.