Mazingira FM

DC Naano:  Serikali wilaya ya Bunda yachukua hatua kuboresha elimu shuleni

3 July 2023, 12:37 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano

Ukosefu wa huduma ya chakula shuleni, miundombinu thabiti chanzo cha utoro na kufeli mitihani kwa wanafunzi

By Edward Lucas

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe. Dkt Vicent Naano amesema serikali wilayani Bunda imechukua hatua mbalimbali kuboresha elimu ikiwa ni pamoja na mpango wa chakula mashuleni.

Hayo ameyabainisha katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Miti Mirefu kata ya Kabarimu halmashauri ya mji wa Bunda alipofika kusikiliza kero za wananchi.

Katika mkutano huo Dkt. Naano amesema tatizo la vibaka na uporaji mdogomdogo unaoendelea  katika mitaa ya Bunda mjini ni kutokana na watoto wanaohitimu shule kutoendelea na masomo badala yake wanabaki maeneo hayo jambo linalopelekea kuanzisha magenge ya uharifu na uvutaji bangi.

Aidha mkuu huyo wa wilaya ameeleza jitihada mbalimbali zilizofanywa na serikali katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na mpango wa chakula shuleni, kuongeza vyumba vya madarasa kupitia fedha zilizotolewa na Mhe Rais kwa shule za sekondari, ujenzi wa madarasa na shule mpya za msingi kupitia mradi wa boost miongoni mwa miradi mingine.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Dkt Vicent Naano

Amesema jitihada hizo zote za serikali zinalenga kuwawezesha watoto wote kupata elimu itakayowasaidia kujikwamua katika mtazamo hasi katika jamii.

Katika mkutano huo amewataka wazazi na walezi kudhibiti utoro wa watoto na kuhakikisha wanawasimamia watoto hao wanafika shuleni.

Wakazi wa Kabarimu wakiwa kwenye mkutano na Mkuu wa Wilaya, Picha na Adelinus Banenwa