Mazingira FM

DC Naano asema wakazi wa Nyatwali watapata haki zao

23 February 2023, 9:22 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda mhe Dkt Vicent Naano amewatoa hofu madiwani  wa Halmashauri ya Mji wa Bunda kuwa hoja zao juu ya suala la Nyatwali wamezichukua na watashauriana na mamlaka husika kuweza kupata muafaka uliyo sahihi.

Mhe Dkt Naano ameyasema hayo  katika baraza maalumu la madiwani  lililoketi leo 22 Feb 2023 ili kujadiri zoezi la kuwahamisha wakazi wa kata ya Nyatwali na namna tathmini inavyofanyiaka .

Katika maelezo yao madiwani wamesema zoezi la Nyatwali bado lina maswali nambayo wananchi wanataka majibu huku wakihoji kwanini baraza hilo tangu mwanzo hawakupewa taarifa rasmi kuhusu serikali kulitwaa eneo la kata ya Nyatwali na utaratibu gani unatumika  na wananchi watalipwa fidia kiasi gani.

Mhe  Dkt Vicent Naano ambaye ni mkuu wa wilaya ya Bunda amesema hoja za madiwani hao ni za msingi hivyo atakaa na timu ya wataalamu wanaohusika na ufanyaji wa tathmini lakini amesisistiza kuwa serikali haiwezi kurudi nyuma juu ya kulitwaa eneo hilo la nyatwali.