Mazingira FM

584 mil, kujenga shule ya sekondari Chamtigiti

22 July 2026, 9:08 pm

Mbunge wa Jimbo la Bunda, Boniface Getere

Baadhi ya miradi ya maendeleo hushindwa kukamilika kwa wakati kutokana na usimamizi hafifu unaofanywa na baadhi ya watumishi wa Serikali.

Na Mariam Mramba

Zaidi ya shilingi milioni 584 zimetolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Chamtigiti  kijiji cha Hunyari, Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Taarifa hiyo imetolewa leo Julai 21, 2026 na  Mkuu wa Kitengo cha  divisheni ya elimu sekondari Halmashauri  ya wilaya ya bunda Bi Pendo Masalu alipokuwa akitambulisha    mradi mpya wa ujenzi wa shule ya sekondari chamtigiti katika mkutano wa wananchi uliohudhuriwa na viongozi wa kijiji ,kata, wataalamu wa halmashauri pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bunda, Boniface Getere.

Sauti ya Pendo Masalu
mkutano wa wananchi na mbunge wa jimbo la Bunda Akizungumza kuhusu ujenzi wa shule mpya ya sekondari

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, George Mbilinyi, amewataka wananchi kuuchukulia mradi huo kuwa mali yao kwa kushiriki katika ulinzi na usimamizi wake.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, George Mbilinyi

Mbunge wa Jimbo la Bunda, Boniface Getere, amesema baadhi ya miradi ya maendeleo hushindwa kukamilika kwa wakati kutokana na usimamizi hafifu unaofanywa na baadhi ya watumishi wa Serikali.

Aidha, amewahimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huo kwa kuchangia nguvu kazi, ikiwemo kuchota maji na kushiriki shughuli nyingine za ujenzi, akisisitiza kuwa Serikali hupeleka miradi kulingana na mahitaji ya wananchi katika maeneo husika.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Bunda, Boniface Getere