Mazingira FM
Mazingira FM
24 August 2026, 6:33 am

Wanafunzi hao wamekanusha taarifa kwamba mwanafunzi huyo alipigwa fimbo mbili pekee, wakidai kuwa alichapwa na walimu kadhaa, huku wakitaja idadi ya takribani walimu 30.
Na Adelinus Banenwa
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makongoro, iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara, wameiomba Serikali kuchukua hatua stahiki dhidi ya walimu wanaodaiwa kumwadhibu mwenzao kwa kumpiga fimbo, hali iliyosababisha kifo chake.
Wakizungumza kuhusu tukio hilo, wanafunzi hao wamekanusha taarifa kwamba mwanafunzi huyo alipigwa fimbo mbili pekee, wakidai kuwa alichapwa na walimu kadhaa, huku wakitaja idadi ya takribani walimu 30.
Aidha, wanafunzi hao wamedai kuwa adhabu hiyo haikuishia kwa mwanafunzi aliyefariki pekee, bali wanafunzi wengine wengi wamekuwa wakikumbana na adhabu kama hiyo shuleni.
Ikumbukwe ni siku mbili tu jeshi la polisi lilithibisha kutokea kwa tukio hilo kupitia kwa kamanda wa polisi mkoa wa Mara Pius Lutumo ambaye alisema hadi sasa walimu sita wanashikiliwa huku ukisubiliwa uchunguzi wa madaktari kujua chanzo hali cha kifo cha mwanafunzi huyo