Mazingira FM

Dampo lawa kero kwa wakazi wa Migungani kata ya Bunda stoo

6 July 2021, 6:35 pm

By Adelinus Banenwa

dampo la maji taka katika Halmashauri ya mji wa Bunda
baadhi ya viongozi wa kata wakiongozwa na diwani wa kata ya bunda stoo wakiangalia ufumbuzi wa dampo katika maeneo ya makazi

Wananchi wa mtaa wa Migungani kata ya Bunda stoo Halmashauri ya Mji wa Bunda wameiomba serikali kuhamisha dampo la Migungani kutokana na kero kubwa wanazozipata

Hayo wameyasema leo july 5, katika eneo la dampo la maji taka wakati wakizungumza na Redio Mazingira FM  wananchi hao wamesema dampo hilo lipo katikati ya makazi ya watu pia shimo la maji taka limejaa

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Bunda stoo Mh Flavian Chacha amesema atawasiliana na serikali pamoja na wataalam wa afya pia kupeleka hoja kwenye baraza la madiwani ili dampo hilo liweze kuhamishwa kwenye makazi ya watu na kutafutiwa sehemu nyingine

Naye afisa afya wa Halmashauri ya Mji wa Bunda  Amani Jumbula amesema uwepo wa dampo hilo ni hatari kwa afya za wananchi hivyo amemuagiza afisa afya wa mtaa kuandika tathimini ya afya ya dampo hilo kama mapenekezo kwenda ofisi ya Mkurugenzi ili kuangalia namna ya kuwasaidia wananchi hao