Mazingira FM

Wawili wapoteza maisha ajali ya gari mkesha wa mwaka mpya Bunda

2 January 2024, 8:55 am

Haice iliyopata ajali, picha na Adelinus Banenwa

Watu wawili wamefariki Dunia na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali iliyotokea usiku wa mkesha wa mwaka mpya eneo la Nyasura makumbusho wilayani Bunda.

Na Adelinus Banenwa

Watu wawili wamefariki Dunia na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali iliyotokea usiku wa mkesha wa mwaka mpya eneo la Nyasura makumbusho wilayani Bunda.

Ajali hiyo imehusisha gari aina ya haice iliyokuwa imebeba kreti za bia na bajaji iliyokuwa imebeba magogo.

bajaji iliyogongwa na haice, picha na Adelinus Banenwa

Moja ya mashuhuda wa ajali hiyo Juma John amesema dereva wa Haice alikuwa na mwendo mkali na taa za gari zilikuwa hafifu sana jambo huwenda hakuweza kuona vizuri mbelepia inaonesha alikuwa amelewa kisha haice hiyo iligonga bajaj iliyokuwa imebeba magogo kwa nyuma kisha kuingia mtaroni .

” kishindo kilikuwa ni kikubwa baada ya haice kuigonga bajaj ilipoteza mwelekeo na kuingia mtaroni watu wawili walifariki hapohapo dereva wa haice na abilia kwenye bajaji”.

Sauti ya shuhuda wa ajali hiyo Juma John

Kwa mujibu wa Afisa mtendaji wa kata ya Nyasura Ndugu Jerrymary Atasasio Kamugisha ameiambia Mazingira Fm kuwa waliopoteza maisha ni Dereva wa Haice Beatus Samsoni aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 32 na 35.

Haice iliyopata ajali, picha na Adelinus Banenwa

Aidha amesema mwingine aliyepoteza maisha alikuwa kwenye bajaji ambaye ametambulika Kwa jina la Omary au Mzuzu miaka 46 mkazi wa mtaa wa Nyerere Bunda mjini huku majeruhi watatu wakiwa wanaendelea kupata huduma kwenye hospital ya DDH Bunda.

Sauti ya Afisa mtendaji wa kata ya Nyasura Ndugu Jerrymary Atasasio Kamugisha