Mazingira FM

Gilyoma: Bunda kutumia mita mpya za maji

4 October 2023, 7:29 pm

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA), Esther Gilyoma. Picha na Catherine Msafiri

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Bunda BUWSSA inatarajia kufunga mita mpya takribani 6000 na kuondoa mita za zamani

Na Catherine Msafiri

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA) Bi. Esther Gilyoma, amesema Mamlaka hiyo inaendelea na utekelezaji wake wa kubadirisha mita zilizokuwepo na kufunga mita mpya ambapo wanatarajia kufunga mita zaidi ya 6000 katika mji wa Bunda
ameeleza hayo leo wakati akizungumza na Mazingira FM ofisini kwake ambapo amesema zoezi la ufungaji wa mita mpya linalenga kuongeza ufanisi wa kupata Ankara ya Maji (Bili) sahihi kulingana na matumizi yako kutokana na kwamba baadhi ya mita tayari zimepoteza uwezo wake hivyo inabidi zibadirishwe.

Gilyoma amewatoa hofu wananchi kuwa ufungwaji wa mita hizo ni bure na hakuna gharama yoyote isipokuwa ushirikiano ndio unaohitajika kwa mteja anayebadirishiwa mita ya zamani na kuwekewa mita mpya.

Sauti ya Esther Gilyoma

Aidha ameeleza kuhusu ufuatiliaji wa wasoma mita kuwa mamlaka inamfuatilia na kuhakiki kuwa amefika sehemu husika na pia wewe kama mteja unapaswa kusoma mita na kuhakiki kile ulichotumiwa kwenye ujumbe wako kupitia simu ya kiganjani kuwa ndicho ulichotumia?

Sauti ya Esther Gilyoma, Mkurugenzi BUWSSA

Katika hatua nyingine ameeleza kuhusu siku Maalum wanayoitenga wao kila mwezi ilikuhamasisha ulipaji wa bili namna ambavyo inasaidia kufanikisha zoezi la ulipaji bili za maji (Makusanyo Day)
pia amewashukuru Wananchi kwa ushirikiano wao mzuri ambapo mpaka sasa Imepanda daraja kutoka C kwenda B kutokana na kuweza kumudu gharama za uendeshaji.

Sauti ya Esther Gilyoma, Mkurugenzi BUWSSA

Hata hivyo kwa sasa Mamlaka inakusanya Mapato yake ya ndani zaidi ya Milioni 150 kwa mwezi .