Mazingira FM

Dallo- watumishi acheni kutumia neno mchakato

2 April 2021, 4:52 pm

Katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Bunda mkoani Mara Ramamdhani Dallo amewataka watumishi wa umma na wakuu wa idara halmasauri ya wilaya ya Bunda kuacha mara moja kutumia neno mchakato na badala yake wajielekeze katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wakati.

Ramamdhani Dallo katibu wa CCM Wilaya ya Bunda

Ametoa maelekezo hayo katika kikao cha baraza la madiwani alipo karibishwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bunda Charles Magafu Manumbu kutoa salamu za chama katika baraza hilo.

Dallo amesema baadhi ya wakuu wa idara wamekuwa namazoea ya kutumia neno mchakato hali inayo pelekea kushindwa kukamilisha miradi ya maendeleo kwa wakati kama ilani ya chama cha Mapinduzi CCM inavyoelekeza.

Aidha Dallo amewaomba watumishi wa umma kushirikiana na waheshimiwa madiwani huku akiwataka madiwani hao kusimamia ipasavyo miradi ya mendeleo.