Mazingira FM

Wakazi wa Bunda watakiwa kutumia wiki ya sheria kupata uelewa wa sheria

29 January 2024, 2:25 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano, mwenye kofia yenye bendera ya Tanzania akiwa na viongozi wengine siku ya uzinduzi wa wiki ya sheria mjini Bunda. Pcha na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano amewataka wananchi wote wilaya ya Bunda kuitumia wiki ya sheria  ili kupata elimu mbalimbali za kisheria.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano amewataka wananchi wote wilaya ya Bunda kuitumia wiki ya sheria  ili kupata elimu mbalimbali za kisheria.

Dc Naano ameyasema hayo katika uzinduzi wa wiki ya sheria wilayani Bunda ambayo imefanyika katika viwanja vya stendi ya zamani mjini Bunda, kauli mbiu mwaka huu ikisema  ’’Umuhimu wa dhana ya haki kwa ustawi wa taifa nafasi ya mahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi wa haki jinai’’.

Naye hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Bunda Mulokozi  Paschal Kamuntu  amewasihi wakazi wa Bunda kujitokeza katika wiki ya sheria kwa kuwa wapo wataalamu mbalimbali kama vile Jeshi la polisi, Mahakimu, Mawakili, Waendesha mashtaka, Takukuru, miongoni mwa wataalamu wengine.

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano, katikati akiwa na hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya ilaya ya Bunda kushoto na katibu tawala Bunda mkono wa kulia pamoja na maafisa wa jeshi la polisi Bunda katika uzinduzi wa wiki ya sheria wilayani Bunda.

Aidha Kamuntu amesema kwa sasa wananchi wamebadilika  tofauti na zamani hasa katika kuhofia mahakama ambapo zamani ilikuwa vigumu kwa wananchi kusogelea ama mahakama au mahakimu lakini kutokana na huduma kusogea karibu nao wamebadilika.

Kamuntu amesema wataalamu wapo kuanzia tarehe 24 mwezi Jan, na tamati au kilele cha siku ya sheria itakuwa tarehe 1 Feb 2024 katika viwanja vya mahakama ya wilaya mjini Bunda.