Mazingira FM

Zito Kabwe kuunguruma Musoma

7 June 2023, 2:12 pm

Chama cha ACT Wazalendo kesho tarehe 8 Juni 2023 kitafanya mkutano mkubwa wa siasa katika viwanja vya shule ya msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.

Hii ikiwa ni mwendelezo wa mikutano yake tangu ilivyozindua mikutano hiyo mwezi Februari 2023 jijini Dar es Salaam baada ya kuruhusiwa kwa mikutano ya kisiasa.

Akizungumza na Radio Mazingira Fm kupitia kipindi cha Asubuhi Leo, Mratibu wa Mikutano na Afisa wa ACT – Wazalendo makao makuu, Ndg. Mussa Bakari ‘ Tembo’ amesema tangu kuondolewa zuio la mikutano ya hadhara chama kimefanya mikutano katika mikoa 9 awamu ya kwanza na sasa katika awamu ya pili watafanya katika mikoa 10.