Mazingira FM

Mkurugenzi Bunda Mji aonya uchafuzi wa mazingira

6 September 2023, 1:07 pm

Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Bunda Emmanuel Mkongo aliyesimama, Picha na Adelinus Banenwa

Mkurugenzi Mkongo amesema wameazimia kutoa maelekezo kwa wafanyabiashara wote hasa wenye maduka kuwa na vitunza taka katika maeneo yao huku wamiliki wa baa na hoteli kuwa na vitunza taka vya aina tatu kwa ajili ya taka ngumu, zinazooza na chupa.

Na Adelinus Banenwa

Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Bunda Emmanuel Mkongo amesema katika mji wa Bunda baadhi ya watu hawazingatii taratibu za usafi wa Mazingira

Mhe Mkongo amesema katika baadhi ya maeneo ya mji wa Bunda baadhi ya wafanyabiashara wanafanya biashara juu ya mitaro ya barabarani ama kwenye hifadhi za barabara wameweka mabanzi juu ya mitaro ya kupitishia maji jambo ambalo ni kinyume na Sheria.

Aidha mkurugenzi Mkongo amesema wameazimia kutoa maelekezo kwa wafanyabiashara wote hasa wenye maduka kuwa na vitunza taka katika maeneo yao huku wamiliki wa baa na hoteli kuwa na vitunza taka vya aina tatu kwa ajili ya taka ngumu, zinazooza na chupa.

Meneja wa TARURA wilaya ya Bunda Eng Baraka Mkuya Picha na Adelinus Banenwa

kwa upande wake meneja wa tarura wilaya ya Bunda Eng Baraka Mkuya amesema kwa mujibu wa sheria ya barabara ya mwaka 2007 inaweka marufuku watu kufanya uchafuzi na uharibifu wa miundombinu ya barabara hasa utupaji wa taka kwenye mitaro.

Eng Baraka ametoa rai kwa wakazi wa Bunda kulinda miundombinu hiyo kwa kuwa atakayebainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake huku akisema faini yakeni kubwa pia waweza kukabilina na kifungo cha hadi miezi sita jela.

sauti ya meneja wa TARURA wilaya ya Bunda Eng Baraka Mkuya