Mazingira FM

Bunda:- Hofu ya mamba na viboko wananchi walazimika kutumia maji ya kwenye madimbwi

5 October 2021, 5:48 pm

wananchi wakifua kando ya dimbwi lililopo bembezoni mwa Barabara

Kutokana na matukio ya mara kwa mara ya wananchi kujeruhiwa au kuuawa na mamba, baadhi ya wananchi wamelazimika kuwa wanatumia maji yaliyotuwama kando kando ya barabara kwa hofu ya kwenda Ziwani au Mtoni kutoka na matukio hayo.

Mazingira Fm imeshuhudia baadhi ya wananchi wakiwa wanafua kwa kutumia maji hayo.

Katika mahojiano na wananchi hao wamesema wamekuwa wakitumia maji hayo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani mfano kufua, kuoga na kupikia hii ni kutokana na hofu ya kwenda mtoni na Ziwani licha ya kuwa wanaishi karibu na mto Rubana.

Ikumbukwe kuwa katika matukio ya hivi karibuni ndani ya miezi minne watu wawili wamepoteza maisha kutokana na kushambuliwa na mamba ambapo mmoja alifariki mto Rubana mwezi June na mwingine amefariki mwezi huu wa October kando ya Ziwa Victoria.

By Edward Lucas