Mazingira FM

Esperanto waadhimisha kuzaliwa Dr. Zamenhof kwa kutembelea pori la Akiba Kijereshi

16 December 2023, 4:04 pm

Wanafunzi wa Sekondari ya Esperanto wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa jumuiya ya Esperanto

Wanafunzi 34 wa shule ya Sekondari Esperanto wakiwa wameambatana na walimu na viongozi wengine wa jumuiya ya Esperanto watembelea pori la Akiba Kijereshi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho kuzaliwa mwanzilishi wa lugha ya Esperanto.

Na Edward Lucas

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Esperanto Wilayani Bunda wameungana na wazungumzaji wengine wa lugha ya Kiesperanto duniani katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa mwanzilishi wa lugha hiyo, Dr Ludovick Zamenhof kwa safari ya utalii pori la akiba la Kijereshi.

Wanafunzi hao wamesema  kupitia safari hiyo wamejifunza vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na maisha ya wanyamapori, ndege, wadudu, mimea na vitu vingine vya kuvutia.

Ashura Ally, mwanafunzi shule ya Sekondari Esperanto akiwa na wanafunzi wengine katika pori la akiba Kijereshi
Sauti ya wanafunzi wa Esperanto

Akizungumzia safari hiyo, Diwani wa Kata ya Ketare ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa jumuiya ya wazungumzaji lugha ya Kiesperanto nchini Tanzania, Mhe. Mramba Simba Nyamkinda amesema hii ni hatua muhimu kwa wanafunzi kutembelea na kujionea maliasili za Tanzania lakini pia kutangaza vivutio vya utalii nchini.

Mhe. Mramba Simba Nyamkinda
Sauti ya Mramba Simba Nyamkinda

Dr L.L. Zamenhof ambaye ni mwanzilishi wa lugha ya Kiesperanto  mnamo miaka ya 1873’s akiamini dunia inaweza kuendelea pasipo vita kwa kusaidiwa na uwepo wa lugha mpya ya kimataifa itakayoweza kuwaunganisha watu wote,

Mwanzilishi huyo alizaliwa tarehe 15 December 1859 sawa na miaka 164 iliyopita na alifariki tarehe 14 April 1917 akiwa na umri wa miaka 58