Mazingira FM

Wakulima watakiwa kulima kilimo hifadhi kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi

14 September 2023, 7:49 pm

Shija Lucas ambaye ni msimamizi wa mpango kilimo hifadhi. Picha na Adelinus Banenwa

Wito umetolewa kwa wakulimakutumia teknolojia ya kilimo hifadhi ili kupata mazao mengi kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayoendelea kushuhudiwa duniani kwa sasa.

Na Adelinus Banenwa

Wito umetolewa kwa wakulimakutumia teknolojia ya kilimo hifadhi ili kupata mazao mengi kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayoendelea kushuhudiwa duniani kwa sasa

Wito huo umetolewa na Shija Lucas ambaye ni msimamizi wa mpango huo kutoka kanisa la AICT MARA  ambapo lengo la mpango huo ni kuwasaidia wakulima kubadili namna ya kulima ikiwa ni pamoja na njia za urutubishaji udongo katika mashamba yao.

Sauti ya Shija kuhusu kilimo hifadhi 
Shija Lucas ambaye ni msimamizi wa mpango kilimo hifadhi. Picha na Adelinus Banenwa

Aidha Ndugu Shija ameeleza kuwa tangu kuanza kwa mpoango huo kumewasaidia kwa kiasi kikubwa wakulima ambapo sehemu ambayo mkulima alikuwa akipata gunia mbili kabla ya kupata elimu ya kilimo hifadhi sasa hivi anapata hadi gunia 10 na kuendelea katika shamba hilohilo.

Sauti ya Shija kuwasaidia wakulima
wakulima kyabakari baada ya kutoka shamba wanajifunza namna ya kuandaa mlo kamili kwa ajili ya familia zao. Picha na Adelinus Banenwa

Kwa upande wao wakulima kutoka kijiji cha Kyabakari wilayani Butiama wamesema wanayaona mabadiliko makubwa tamgu waanze kutumia teknolojia ya  kilimo hifadhi ukilinganisha na mwanzo hasa katika upande wa mavuno kwenye zao la mahindi.

Sauti ya mkulima mnufaika