Mazingira FM
Mazingira FM
19 April 2026, 6:23 am

Wakati mwingine hupokea simu watu wakitaka kujiunga na freemason, matusi ya nguoni au wakati mwingine habari za uongo kuhusu matukio ya maokozi.
Na Adelinus Banenwa
Imeelezwa kuwa changamoto ya miundombinu, kutotolewa taarifa mapema na taarifa zisizo sahihi bado ni changamoto kwa jeshi la zimamoto na uokoaji wilaya ya Bunda.
Hayo yameelezwa leo April 18, 2026 na maafisa wa zimamoto na uokoaji kutoka wilaya ya bunda kupitia kipindi cha ufahamu wa sheria kinachorushwa radio mazingira.
Maafisa hao wamesema wakati mwingine hupokea simu watu wakitaka kujiunga na freemason, matusi ya nguoni au wakati mwingine habari za uongo kuhusu matukio ya maokozi hali inayo onekana kama changamoto kwao.
Mkaguzi msaidizi wa zimamoto na uokoaji wilaya ya Bunda DFO Dikson Joseph Madale na CPL Magesa Dismas wamesema miongoni mwa majukumu ya zimamoto na uokoaji ni Pamoja na kutoa elimu kwa jamii namna ya kujilinda dhidi ya majanga mbalimbali ikiwemo ajali za moto, kuzama kwenye madimbwi, ziwani au kwenye visima miongoni mwa mengine.
Aidha wametoa wito kwa jamii kuzingatia ushauri unaotolewa na maafisa wa zimamoto na uokoaji ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza ikiwemo, watu kuvaa majaketi okozi wakiwa ziwani, kulinda Watoto wasichezee kwenye madimbwi na kutumia namba 114 ili kutoa taarifa za maokozi.