Mazingira FM

WWF watua kwenye kitalu cha miti cha WUAs-Butiama

29 September 2023, 12:21 pm

Wataalamu wa WWF wakiwa wametembelea kitaku Cha miti WUAs Kijiji cha Kwisaro Wilaya ya Butiama. Picha na Thomas Masalu

Na Thomas Masalu

Watalaamu wa WWF wametembelea kitalu cha miti cha Jumuiya ya watumia maji ya mto Mara kusini ( WUAs) kilichopo Kijiji cha Kwisaro kata ya Nyamimange wilaya ya Butiama katika lengo la kujionea shughuli zinavyoendelea katika utunzaji wa Mazingira na vyanzo vya maji kwenye eneo hilo.

Kitalu cha miche chini ya ufadhili WWF katika kijiji cha Kwisaro Wilaya ya Butiama. Picha na Thomas Masalu

Kitalu hicho kimefadhiliwa na shirika la WWF katika kuwajengea uwezo wana Jumuiya hao, miche ya miti, viriba ya miche ya miti, tanki la maji, uzio na kuwatengenezea kitalu chenyewe.

Akizungumza na Mazingira fm, Mwenyekiti wa jumuiya hiyo ya watumia maji ya mto Mara kusini, ndugu Mairi Magabe ameshukuru shirika la WWF katika kuwasaidia kila hatua ambapo katika msimu huu wamezalisha jumla ya Miche elfu therathini na nne pekee.

Pamoja na hayo Magabe amesema wamezalisha Miche hiyo kutokana na changamoto ya soko hivyo inawalazimu kuzalisha Miche michache kuendana na soko la miche hiyo.

Aidha Magabe amesema jamii ya eneo hilo wana mwitikio mkubwa wa kuhifadhi mazingira lakini changamoto inayowakabili ni kuwa wagumu kutoa pesa wenyewe kununua miche ya miti hivyo husubili miche ya misaada ambapo ikipatikana huisha mara moja.

Sauti ya Mairi Magabe, Mwenyekiti wa WUAs