Mazingira FM

Kesi yatajwa kuchelewesha wakazi wa Nyatwali kuhama

6 September 2023, 1:26 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vincent Naano, Picha na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vincent Naano amesema mchakato wa kuwaamisha wakazi wa Nyatwali huwenda ukakamilika mwishoni mwa mwezi wa tisa.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vincent Naano amesema mchakato wa kuwaamisha wakazi wa Nyatwali huwenda ukakamilika mwishoni mwa mwezi wa tisa.

Dkt Naano ameyasema hayo katika kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya mji wa Bunda katika kikao Cha robo ya nne ya mwaka 2022 na 2023 yaani April na June.

Mhe mkuu wa wilaya amesema changamoto iliyosababisha mchakato huo kuchelewa ni pamoja na kesi iliyofunguliwa mahamani ikiwashitaki Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Bunda, mkuu wa wilaya ya Bunda, mkuu wa mkoa wa Mara, mwanasheria mkuu wa serikali, wizara ya maliasili na utalii pamoja na TAMISEMI.

Aidha Mhe Naano amesema changamoto nyingine ni watu kuwa na hati feki pamoja na watu kujiongezea maeneo ambapo eneo la Nyatwali lina ukubwa wa kilometa za mraba 14 elfu lakini hadi Sasa kupitia tathmini ya tayari eneo la Nyatwali limefikia kilometa za mraba elfu 16.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vincent Naano
Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vincent Naano
Sauti ya diwani wa kata ya Nyatwali Malongo Mashimo Picha na Adelinus Banenwa

Kwa upande wake Mhe diwani wa kata ya Nyatwali Malongo Mashimo amesema wao kama wananyatwali hawana tatizo na serikali itawalipa lini bali huduma mbalimbali za kijamii zilizositishwa Kwa wakazi hao serikali inachukua hatua gani.

Diwani wa kata ya Nyatwali Malongo Mashimo