Mazingira FM

Tamau: kamati yasiasa yakaa nakuamua

28 September 2021, 1:15 pm

Matale kikoi mwenyekiti wa CCM tawi la tamau

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho Mwenyekiti wa CCM tawi la Tamau, Matale Kikoi amesema ni kwa muda sasa kumekuwa hakuna mahusiano mazuri kati ya viongozi wa chama na serikali katika mtaa wa Tamau jambo linalokwamisha utekeleza wa shughuli za maendeleo katika eneo hilo.

Amesema licha ya kuwako na hali hiyo kwa muda sasa wao kama viongozi wamekuwa hawaoni mipango mikakati yoyote inayowekwa ili kuondoa hali hiyo, hivyo wao kama Kamati ya Siasa wameamua kuwa na kikao hicho ili kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.

Maona Kawege katibu wa CCM tawi la tamau

Kwa upande wake Katibu wa ccm Tawi la Tamau, Maona Kawege amesema kumekuwa na hali ya sintofahamu kuibuka mara kwa mara pindi viongozi wa chama wanapohoji utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika mtaa huo jambo linalodhoofisha nguvu ya chama katika usimamizi wa shughuli za maendeleo na kujiona kama wao hawana nguvu ya kuhoji.

Katika majadiliano hayo Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Tamau, Asafu Ernest Owiti amepongeza hatua ya kuitisha kikao hicho lakini pia ametumia nafasi hiyo kuonesha malalamiko yake kwa baadhi ya viongozi kutoshirikishwa katika kikao hicho

Aidha kuhusu baadhi ya tuhuma kuhusu viongozi wa chama kutoshirikishwa katika shughuli za maendeleo amesema baadhi ya viongozi wamekuwa hawafiki katika vikao. Akitolea mfano kikao cha kusoma mapato na matumizi jana tarehe 27 September 2021 ni wajumbe wasiozidi watatu tu kutoka kwenye kamati hiyo ndio walioudhuria.

By Edward Lucas