Mazingira FM

IRINGA : Wahariri wa redio za kijamii Nchini wanolewa kushiriki vyema sensa ya watu na makazi 2022

16 June 2022, 5:08 pm

*IRINGA*

Mmoja ya watoa Mada kwenye mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari vya kijamii Tanzania yaliyofanyika 2022

Mtandao wa redio za kijamii Tanzania TADIO kwa kushirikiana na ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS wamefanya mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari vya kijamii nchini kwa lengo la kuwawezesha kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa zoezi la sensa ya watu na makazi mwaka 2022

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari vya kijamii Tanzania *HELLEN SIRIWA Mtaalamu wa idadi ya watu kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu* amesema lengo kuu la sensa ya watu na makazi ni kujua idadi ya watu ili kusaidia serikali kupanga mipango ya maendeleo kwa watu wake ambapo sensa ya Tanzania inajikita katika dhana kuu tatu ambazo ni kiuchumi, kijamii na Mazingira

Aidha amebainisha kuwa sensa ya mwaka 2022 itakuwa sensa ya 6 tangu nchi ya Tanzania iwe Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo sensa ya kwanza ilifanyika 1967

Kwa upande wake *Amina Ramadhani msanifu majengo mkuu* kutoka wizara ya Ardhi amesema wizara hiyo kwa kushirikiana na ofisi ya Taifa ya Takwimu wanaendesha zoezi la sensa ya majengo ili kuandaa kanzidata kwa ajili ya maendeleo ya Taifa

Bi Amina Ameongeza kuwa tofauti na sensa zingine sensa ya mwaka huu itahusisha majengo ili kutaka kujua umiliki wa jengo, hali ya jengo, shughuli Gani inafanyika katika jengo husika miongoni mwa mambo mengine

Pia sensa ya mwaka huu itahusisha Anwani za makazi ambapo ni zoezi linaloendelea nchini

by Adelinus Banenwa