Mazingira FM

Bajeti Bunda DC 2024 na 2025 ni zaidi ya bilioni 31.3

21 February 2024, 9:28 pm

Mwenyekiti wa halamshauri ya wilaya ya Bunda Mhe Charles Magafu Manumbu, Picha na Adelinus Banenwa

Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara tarehe 20 Feb, 2024 limeidhinisha makadirio ya bajeti ya mapato na matumizi ya zaidi ya shilingi bilioni 31.3 kwa mwaka wa fedha 2024 na 2025.

Na Adelinus Banenwa

Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara leo tarehe 20 Feb, 2024 limeidhinisha makadirio ya bajeti ya mapato na matumizi ya zaidi ya shilingi bilioni 31.3 kwa mwaka wa fedha 2024 na 2025.

Waheshimiwa madiwani Bunda DC wakifuatilia maelekezo ya mwenyekiti wa halamshauri, Picha na Adelinus Banenwa

Akisoma makadirio hayo mbele ya waheshimiwa madiwani, mwenyekiti wa halamshauri ya wilaya ya Bunda Mhe Charles Magafu Manumbu amesema kati ya fedha hizo mapato ya ndani ni zaidi ya bilioni 2, za serikali kuu ni zaidi ya  shilingi bilion 28 .

Aidha Mhe Manumbu amesema katika fedha hizo bilioni 18 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi, bilioni 8 miradi ya maendeleo na zaidi ya bilion 1.3 ni kwa ajili ya matumizi mengine.