Mazingira FM

Ukiibiwa au kupoteza mali toa taarifa polisi

13 May 2026, 10:20 am

Jonas Kaijage Msaidizi wa mkuu wa polisi jamii wilaya ya Bunda.

Utoaji wa taarifa za wizi au upotevu wa mali inasaidia kuwakamata watuhumiwa mapema.

Na Adelinus Banenwa

Wito umetolewa kwa wananchi kujenga utamaduni wa kutoa taarifa pindi wanapopoteza mali zao au kuibiwa ili kurahisisha uchunguzi wa matukio ya kihalifu.

Akizungumza kupitia kipindi cha Asubuhi leo kinachorushwa kupitia Radio Mazingira fm Jonas Kaijage Msaidizi wa mkuu wa polisi jamii wilaya ya Bunda amesema ni wajibu wa mwananchi pindi anapopoteza mali yake au kuibiwa kutoa taarifa polisi lengo likiwa ni kuweka kumbukumbu za uhalali wa mali hiyo.

Pia kaijage ameongeza kuwa utoaji wa taarifa za wizi au upotevu wa mali inasaidia kuwakamata watuhumiwa mapema pia ukichelewa kutoa taarifa inaweza ikapelekea kupoteza haki yako ya umiliki wa mali husika au mali hiyo kutumika kufanya uhalifu.