Mazingira FM

BUFADESO, Butiama DC wapanda miti 1000 siku ya mazingira

5 June 2026, 8:03 pm

Zoezi la upandaji miti katika eneo la kituo cha afya kukirango ikiwa ni siku ya mazingira duniani

Jumla ya miti 1,000 imepandwa  katika kituo cha afya cha kukirango  pamoja na ofisi za halmashauri ya wilaya ya Butiama.

Na Adelinus Banenwa

Katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, jumla ya miti 1,000 imepandwa  katika kituo cha afya cha kukirango  pamoja na ofisi za halmashauri ya wilaya ya Butiama

Miti hiyo imepandwa na Shirika la Bufadeso kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya Butiama pamoja na wananchi kama sehemu ya juhudi za kuhifadhi mazingira na kujenga Tanzania ya kijani.

Afisa miradi kutoka shirika la BUFADESO Victor Uromi

Akizungumza katika maadhimisho hayo afisa miradi kutoka shirika la BUFADESO Victor Uromi amesema katika miti 1000 iliyopandwa ipo miti yam bao, matunda na vivuli pia imekuwa nafasi ya utoaji elimu kwa jamii namna ya kupanda miti ikiwa ni pamoja na nafasi kati ya mti mmoja na mwingine, ukubwa wa shimo, na aina ya miti inayotakiwa kupandwa.

Afisa miradi kutoka shirika la BUFADESO Victor Uromi
Mmoja wa wananchi waliojitokeza kwenye zoezi la upandaji miti likiongozwa na BUFADESO maadhimisho siku ya mazingira Duniani

Adon Nyanzagi afisa kutoka halmashauri ya wilaya ya Butiama amesema zoezi la upandaji miti halifanyiki tu siku ya mazingira bali umekuwa ni utamaduni wa halmashauri hiyo kupanda miti katika taasisi zake kama vituo vya afya na shule pia wamekuwa wakiweka vyanzo vya maji ili kuhakikisha miti hiyo inapata maji ili iendelee kustawi.

Sauti ya Adon Nyanzagi afisa kutoka halmashauri ya wilaya ya Butiama
Mwenyekiti wa BUFADESO akipanda mti

Kwa upande wao wananchi walioshiri katika zoezi la upandaji miti wameipongeza BUFADESO kwa kuendelea kutoa elimu ya upandaji miti na faida zake kwenye jamii pia wameeleza juu ya shirika hilo kuendelea kutoa miti bure kwenye taasisi  ambapo wameahidi kuendelea kuhamasisha wananchi wengine kuwa na udamaduni wa kupanda miti kwa lengo la kulinda mazingira na kudhibiti Athari za mabadiriko ya tabia nchi.

Sauti za wananchi