Mazingira FM

Mkandarasi wa usafi atimuliwa Bunda kwa kushindwa kazi

17 February 2024, 10:06 pm

Afisa utumishi Halmashauri ya Mji wa Bunda, Picha na Adelinus Banenwa

Halmashauri ya mji wa Bunda imetangaza kuvunja mkataba na mkandarasi wa usafi ndani ya mji wa Bunda kutokana na kushindwa kutekeleza mkataba wake.

Na Adelinus Banenwa

Halmashauri ya mji wa Bunda imetangaza kuvunja mkataba na mkandarasi wa usafi ndani ya mji wa Bunda kutokana na kushindwa kutekeleza mkataba wake.

Ufafanuzi huo umetolewa na Protas Majula afisa mazingira na usafi halmashauri ya mji wa Bunda katika mkutano wa hadhara wa ofisi ya mkurugenzi kusikiliza kero za wananchi kata ya Nyasura.

Majula amesema mkandarasi aliyekuwepo (MAGEREZA) alimaliza muda wake mwezi wa saba mwaka jana na hakuomba tena, huku  kampuni iliyotuma maombi na kupata kandarasi hiyo imeonekana haina uwezo wa kuhudumia mji wa Bunda hivyo  halmashauri imelazimika kuvunja mkataba na mkataba huo unakoma Feb 29, 2024 na tayari halmashauri imeshapata mkandarasi mwingine wa kufanya usafi mjini Bunda.

Diwani wa kata ya nayasura Magigi Samweli Kiboko, Picha na Adelinus Banenwa

Diwani wa kata ya nayasura Magigi Samweli Kiboko amesema kile wanachokililia wananchi kuhusu mkandarasi wa usafi kweli ni changamoto na tayari kupitia baraza la madiwani walimuelekeza mkurugenzi kuchukua hatua kwa mkandarasi huyo kwa kuwa amekosa sifa na ameshindwa kazi,

Baadhi ya wakazi wa nyasura waliyofika kwenye Mkutano, Picha na Adelinus Banenwa

Awali wananchi wa kata ya nyusura mbele ya  Afisa utumishi aliyemuwakilisha  Mkurugenzi walitoa  malalamiko yao juu ya  suala mkandarasi wa usafi kushindwa kazi  jambo linalosababisha uchafu kuzagaa kila kona ndani ya mji wa Bunda.